An-Naml 27:65
النملقُل لَّا يَعْلَمُ مَن فِى ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضِ ٱلْغَيْبَ إِلَّا ٱللَّهُ ۚ وَمَا يَشْعُرُونَ أَيَّانَ يُبْعَثُونَ
Sema: Hapana katika mbingu na ardhi ajuaye ya ghaibu isipokuwa Mwenyezi Mungu. Wala wao hawajui lini watafufuliwa.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Sema: Hapana katika mbingu na ardhi ajuaye ya ghaibu isipo kuwa Mwenyezi Mungu. Wala wao hawajui lini watafufuliwa. [65]
[65] Sema, ewe Mtume: Hakika mwenye kutenda yote haya peke yake ndiye Yeye Subhanahu aliye tengeka peke yake kwa kuyajua mambo ya ghaibu yalioko mbinguni na duniani. Na Yeye huyo ndiye Mwenyezi Mungu wa pekee. Wala watu hawajui wakati gani watafufuliwa kutoka makaburini kwao kwa ajili ya kuhisabiwa na kulipwa.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Sema, ewe Mtume, kuwaambia wao, «Hakuna yoyote ajuwaye, mbinguni wala ardhini, jambo lolote lililofichika ambalo Allah Mtukufu Amejihusisha Mwenyewe kulijua. Na wao hawajui ni lini watafufuliwa kutoka makaburini mwao wakati wa Kiyama kusimama».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net