Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 27 · Aya ya 63

An-Naml 27:63

النمل

أَمَّن يَهْدِيكُمْ فِى ظُلُمَـٰتِ ٱلْبَرِّ وَٱلْبَحْرِ وَمَن يُرْسِلُ ٱلرِّيَـٰحَ بُشْرًۢا بَيْنَ يَدَىْ رَحْمَتِهِۦٓ ۗ أَءِلَـٰهٌ مَّعَ ٱللَّهِ ۚ تَعَـٰلَى ٱللَّهُ عَمَّا يُشْرِكُونَ

Maana

Au ni nani yule anayewaongoa katika giza la bara na bahari, na akazipeleka pepo kuleta bishara kabla ya rehema zake? Je, yupo mungu pamoja na Mwenyezi Mungu? Ametukuka Mwenyezi Mungu juu ya hao wanaomshirikisha nao.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Au nani yule anaye kuongoeni katika giza la bara na bahari, na akazipeleka pepo kuleta bishara kabla ya rehema zake? Je! Yupo mungu pamoja na Mwenyezi Mungu? Ametukuka Mwenyezi Mungu juu ya wanao washirikisha naye. [63]

[63] Bali waulize, ewe Mtume: Nani anaye waongoza katika nyendo za katika giza la usiku katika safari za nchi kavu na baharini? Na nani anaye zipeleka pepo zinazo bashiria mvua, nayo ni rehema itokayo kwa Mwenyezi Mungu? Je! Yupo mungu pamoja na Mwenyezi Mungu anaye fanya hayo? Mwenyezi Mungu Subhanahu ametakasika kuwa na mshirika.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Je, kuviabudu vile mnavyomshirikisha navyo Allah Mtukufu ni bora au Yule Anayewaongoza katika giza la bara na bahari mnapopotea na njia ikawa na giza kwenu, Ambaye Anapeleka upepo wenye kutoa bishara njema ya kile ambacho Allah Mtukufu Anawarehemu waja Wake kwacho, nacho ni mvua yenye kuhuisha ardhi iliyokufa? Je, kuna muabudiwa yoyote pamoja na Allah Mtukufu anayewafanyia chochote katika hayo mkamuomba badala yake? Ameepukana Allah Mtukufu na kutakasika na hivyo ambavyo wao wanamshirikisha navyo asiyekuwa Yeye.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

An-Naml

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net