An-Naml 27:58
النملوَأَمْطَرْنَا عَلَيْهِم مَّطَرًا ۖ فَسَآءَ مَطَرُ ٱلْمُنذَرِينَ
Na tukawanyeshea mvua. Basi ni ovu mno mvua hiyo ya wale waliokwisha onywa.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na tukawanyeshea mvua. Ni ovu kweli kweli hiyo mvua ya walio kwisha onywa. [58]
[58] Na Sisi tukawanyeshea mvua hao mafisadi, mvua ya adhabu na nakama. Ilikuwa mvua ya kuwahiliki walio onywa kuwa watapata adhabu chungu, na wala wasisikie.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na tukawateremshia kutoka mbinguni mvua ya mawe ya udongo yenye kuangamiza. Ilikuwa mbaya mno mvua ya hao walioonywa ambao hoja iliwasimamia.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net