Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 27 · Aya ya 56

An-Naml 27:56

النمل

فَمَا كَانَ جَوَابَ قَوْمِهِۦٓ إِلَّآ أَن قَالُوٓا۟ أَخْرِجُوٓا۟ ءَالَ لُوطٍ مِّن قَرْيَتِكُمْ ۖ إِنَّهُمْ أُنَاسٌ يَتَطَهَّرُونَ

Maana

Basi haikuwa jawabu ya kaumu yake isipokuwa ni walisema, "Wafukuzeni wafwasi wa Luti kutoka katika mji wenu. Hakika wao ni watu wanaojitia usafi."

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Basi haikuwa jawabu ya watu wake ila ni kusema: Wafukuzeni wafwasi wa Luut'i katika mji wenu. Hao ni watu wanao jitia usafi. [56]

[56] Haikuwa jawabu ya watu wake alipo wakataza ila ni kusema: Mtoleeni mbali Luut'i na wafwasi wake katika mji huu. Kwani wao wanajitakasa hawataki kushirikiana nasi katika haya tuyatendayo.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Watu wa Lûṭ hawakuwa na jawabu la kumpa isipokuwa ni kuambiana wao kwa wao, «Watoeni wafuasi wa Lûṭ kwenye mji wenu, kwani wao ni watu wanaojiepusha na kuwaendea wanaume.» Waliwaambia hilo kwa njia ya kuwafanyia shere.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

An-Naml

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net