Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 27 · Aya ya 50

An-Naml 27:50

النمل

وَمَكَرُوا۟ مَكْرًا وَمَكَرْنَا مَكْرًا وَهُمْ لَا يَشْعُرُونَ

Maana

Basi wakapanga mipango yao, na Sisi tukapanga mipango yetu, na wao hawatambui.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Basi wakapanga mipango yao, na Sisi tukapanga mipango yetu, na wao hawatambui. [50]

[50] Walipanga kumuuwa Swaleh na ahali zake, na Mwenyezi Mungu nyuma yao kapanga kumwokoa Nabii wake na ahali zake, na kuwateketeza wao, na hali wao hata hawatambui.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Basi wakazipanga hila hizi za kumuangamiza Ṣãliḥ na watu wake kwa kuwafanyia vitimbi, tukamuokoa Nabii wetu Ṣãliḥ, amani imshukie, na tukawapatiliza kwa mateso kwa ghafla na hali wao hawatazamii vitimbi vyetu kwao kama malipo ya vitimbi vyao.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

An-Naml

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net