Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 27 · Aya ya 44

An-Naml 27:44

النمل

قِيلَ لَهَا ٱدْخُلِى ٱلصَّرْحَ ۖ فَلَمَّا رَأَتْهُ حَسِبَتْهُ لُجَّةً وَكَشَفَتْ عَن سَاقَيْهَا ۚ قَالَ إِنَّهُۥ صَرْحٌ مُّمَرَّدٌ مِّن قَوَارِيرَ ۗ قَالَتْ رَبِّ إِنِّى ظَلَمْتُ نَفْسِى وَأَسْلَمْتُ مَعَ سُلَيْمَـٰنَ لِلَّهِ رَبِّ ٱلْعَـٰلَمِينَ

Maana

Akaambiwa: Liingie behewa la hili jumba. Alipoliona, alidhani ni maji, na akapandisha nguo mpaka kwenye miundi yake. (Suleiman) akasema: Hakika hilo ni behewa lililofanyiwa sakafu ya vioo! Akasema (Malkia): Mola wangu Mlezi! Hakika mimi nimejidhulumu, na sasa ninanyenyekea pamoja na Suleiman kwa Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa walimwengu wote.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Akaambiwa: Liingie behewa la hili jumba. Alipo liona alidhani ni maji, na akapandisha nguo mpaka kwenye miundi yake. (Sulaiman) akasema: Hakika hilo ni behewa lilio sakafiwa kwa viyoo! Akasema (Malkia): Mola wangu Mlezi! Mimi nimejidhulumu nafsi yangu, na sasa nanyenyekea pamoja na Sulaiman kwa Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa walimwengu wote. [44]

[44] Baada ya hao akaambiwa: Ingia katika jumba la Sulaiman. Na uwanja wake wa ndani ulikuwa umesakafiwa kwa kiyoo, na chini yake maji, na samaki wakiogelea humo. Kupandisha nguo miundi yake ya miguu ikaonekana, kwa kuwa alidhania ni maji. Sulaiman akamwambia hicho ni kiyoo, basi yakamuathiri yale madhaahiri ya kilimwengu, na akaona kuwa ufalme wake yeye haufai chochote mbele ya ufalme wa Nabii Sulaiman. Akasema: Mola Mlezi! Hakika mimi nimeidhulumu nafsi yangu kwa kughurika na ufalme wangu na ukafiri wangu. Na sasa ninanyenyekea pamoja na Sulaiman kumuamini Mwenyezi Mungu Mtukufu, Mwenye kuumba walimwengu wote na kuwalea na kuwasimamia.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Akaambiwa, «Ingia kwenye jumba.» na ukumbi wake ulikuwa wa ukoa, chini yake palikuwa na maji. Alipouona ukumbi alidhania ni maji yanayopiga mawimbi, na akafunua miguu yake ili kuingia majini. Sulaymān akamwambia, «Huo ni ukumbi laini wa ukoa ulio safi na maji yako chini yake.» Akatambua ukubwa wa ufalme wa Sulaymān na akasema, «Mola wangu! Nimeidhulumu nafsi yangu kwa ushirikina niliokuwa nao, na nimesalimu amri kwa kumfuata Sulaymān kwa kuingia kwenye dini ya Mola wa viumbe wote».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

An-Naml

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net