Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 27 · Aya ya 42

An-Naml 27:42

النمل

فَلَمَّا جَآءَتْ قِيلَ أَهَـٰكَذَا عَرْشُكِ ۖ قَالَتْ كَأَنَّهُۥ هُوَ ۚ وَأُوتِينَا ٱلْعِلْمَ مِن قَبْلِهَا وَكُنَّا مُسْلِمِينَ

Maana

Basi (Malkia) alipofika akaambiwa: Je, kiti chako cha enzi ni kama hiki? Akasema: Kama kwamba ndicho hiki. (Suleiman na watu wake wakasema): Na sisi tumepewa elimu kabla yake (Malkia), na tukawa Waislamu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Basi (Malkia) alipo fika akaambiwa: Je! Kiti chako cha enzi ni kama hiki? Akasema: Kama kwamba ndicho hichi. (Sulaiman na watu wake wakasema): Na sisi tumepewa ilimu kabla yake (Malkia), na tukawa Waislamu. [42]

[42] Alipo fika jicho lake lilipiga kwenye kiti chake cha enzi. Akaambiwa: Je! Kiti chako cha enzi ni mfano wa hiki? Akasema kwa vile kilivyo kamilika kufanana: Kama kwamba ndicho hichi. Na Sulaiman na walio pamoja naye wakasema: Sisi tulisha pewa ujuzi kumjua Mwenyezi Mungu na uwezo wake na ukweli wa yaliyo kuja kutoka kwake kama anavyo jua mwanamke huyu. Na sisi tangu hapo ni watu tulio mfuata Mwenyezi Mungu na tunamsafia Yeye ibada.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Alipokuja malkia wa Saba’ kwa Sulaymān kwenye kikao chake aliambiwa, «je, kitanda cha ufalme wako kiko hivi?» Akasema, «Hicho kinafanana nacho.» Ikambainikia Sulaymān kuwa amejibu jawabu la sawa na ameshajua uwezo wa Allah Mtukufu na usahihi wa unabii wa Sulaymān, amani imshukie. Na tulipewa elimu ya kumjua Allah Mtukufu na kujuwa uwezo Wake kabla yake yeye, na tulikuwa ni wenye kuifuata amri ya Allah Mtukufu ni wenye kuifuata dini ya Uislamu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

An-Naml

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net