An-Naml 27:37
النملٱرْجِعْ إِلَيْهِمْ فَلَنَأْتِيَنَّهُم بِجُنُودٍ لَّا قِبَلَ لَهُم بِهَا وَلَنُخْرِجَنَّهُم مِّنْهَآ أَذِلَّةً وَهُمْ صَـٰغِرُونَ
Rejea kwao! Kwa yakini sisi tutawajia kwa majeshi wasioyaweza kuyakabili. Na hakika tutawatoa humo na hali wao wamekuwa madhalili na wanyonge.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Rejea kwao! Kwa yakini sisi tutawajia kwa majeshi wasio yaweza kuyakabili. Na hakika tutawatoa humo na hali wao wamekuwa madhalili na wanyonge. [37]
[37] Akasema, akimsemeza yule msemaji kwa jina lao: Ewe mjumbe! Rejea kwao. Wallahi! tutawatokea kwa majeshi wasio yaweza kupambana nayo na kuyakabili. Na tutawatoa kwenye nchi ya Sabai nao wamepoteza utukufu wao, wamefanywa watumwa.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na Sulaymān, amani imshukie, akasema kumwambia mjumbe wa watu wa Saba’, «Rejea kwao, kwani naapa kwa Allah Mtukufu, tutawajia na askari ambao watu wa saba’ hawataweza kupambana nao na kukabiliana nao, na tutawatoa kutoka nchini mwao wakiwa wadhalilifu, hali ya kuwa wanyonge wenye kudharauliwa, iwapo hawatafuata Dini ya Allah Mtukufu Peke Yake na hawataacha kumuabudu asiyekuwa Yeye».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net