Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 26 · Aya ya 86

Ash-Shu'araa 26:86

الشعراء

وَٱغْفِرْ لِأَبِىٓ إِنَّهُۥ كَانَ مِنَ ٱلضَّآلِّينَ

Maana

Na umsamehe baba yangu, kwani hakika alikuwa miongoni mwa wapotovu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na umsamehe baba yangu, kwani hakika alikuwa miongoni mwa wapotovu. [86]

[86] Na mjaalie baba yangu astahili msamaha kwa kumwezesha kuwa Muislamu. Na yeye alikuwa kamuahidi kusilimu siku alio achana naye, kwani yeye huyo baba alikuwa ameitupa kando njia ya uwongofu na uwongozi.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hii ni dua ya Ibrãhîm, amani imshukie, ya kumuomba Allah Mtukufu Amuokoe babake na upotevu na Ampe uongofu, ili Amsamehe, kama Ibrãhîm alivyomuahidi baba yake kumuombea kwa mungu, na ilipomdhihirikia kuwa yeye ni mwenye kuendelea kwenye ukafiri na ushirikina mpaka afe alijiepusha naye.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Ash-Shu'araa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net