Ash-Shu'araa 26:77
الشعراءفَإِنَّهُمْ عَدُوٌّ لِّىٓ إِلَّا رَبَّ ٱلْعَـٰلَمِينَ
Kwani hakika hao ni adui zangu, isipokuwa Mola Mlezi wa walimwengu wote.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Kwani hakika hao ni adui zangu, isipo kuwa Mola Mlezi wa walimwengu wote. [77]
[77] Kwani hakika hao mnao waabudu badala ya Mwenyezi Mungu ni maaadui kwangu mimi na kwenu. Basi mimi siwaabudu hao. Lakini ninaye muabudu na najijongeza kwake ni Muumba wa walimwengu wote, na Mwenye kumiliki mambo yao, na Mwenye kuwalinda.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Kwani hao mnaowaabudu badala ya Allah Mtukufu ni maadui zangu. Lakini Mola wa viumbe wote na Mmiliki wa mambo yao, Yeye Peke Yake Ndiye ninayemuabudu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net