Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 26 · Aya ya 5

Ash-Shu'araa 26:5

الشعراء

وَمَا يَأْتِيهِم مِّن ذِكْرٍ مِّنَ ٱلرَّحْمَـٰنِ مُحْدَثٍ إِلَّا كَانُوا۟ عَنْهُ مُعْرِضِينَ

Maana

Wala hauwafikii ukumbusho mpya kutoka kwa Arrahman (Mwingi wa rehema), isipokuwa wao huupa mgongo.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Wala hauwafikii ukumbusho mpya kutoka kwa Arrahman ila wao hujitenga nao. [5]

[5] Wala Mwenyezi Mungu hawaletei watu wako kwa ufunuo wake ya kuwakumbusha Dini ya Haki kuwa ni rehema kwao, ila wao huzua upya upinzani na ukafiri kuukataa. Kwani njia ya uwongofu imekwisha zibwa mbele yao.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na hauwajii washirikina hawa ukumbusho, kutoka kwa Mwingi wa rehema unaoanzwa kuteremshwa, kitu baada ya kitu, wenye kuwaamrisha na kuwakataza na kuwakumbusha Dini ya kweli, isipokuwa wanaupa mgongo na hawaukubali. 1 Rejea sura ya Al-Baqarah aya:3, kwa maelezo zai

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Ash-Shu'araa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net