Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 26 · Aya ya 224

Ash-Shu'araa 26:224

الشعراء

وَٱلشُّعَرَآءُ يَتَّبِعُهُمُ ٱلْغَاوُۥنَ

Maana

Na watungaji mashairi ni wapotovu ndio wanawafuata.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na watungaji mashairi ni wapotofu ndio wanawafuata. [224]

[224] Makafiri wanasema: Hii Qur'ani ni mashairi, na Muhammad ni mtungaji mashairi. Mwenyezi Mungu ameyavunja haya kwa kuthibitisha kuwa hakika Qur'ani imejaa hikima na hukumu. Mpango wake unapingana na mpango wa mashairi ambao unategemea juu ya kweli na uwongo. Na amebainisha kwamba hali ya Muhammad s.a.w. inapingana na hali ya watungaji mashairi. Yeye anasema kwa hikima, wao wanasema kwa udanganyifu. Na hii ndiyo hali ya wengi katika watungaji mashairi.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na washairi, mashairi yao yanasimama juu ya ubatilifu na urongo, na wanafuatana na wao wapotevu waliopotoka kama wao.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Ash-Shu'araa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net