Ash-Shu'araa 26:22
الشعراءوَتِلْكَ نِعْمَةٌ تَمُنُّهَا عَلَىَّ أَنْ عَبَّدتَّ بَنِىٓ إِسْرَٰٓءِيلَ
Na hiyo ndiyo neema ya kunisimbulia, na wewe umewatia utumwani Wana wa Israili?
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na hiyo ndiyo neema ya kunisumbulia, na wewe umewatia utumwani Wana wa Israili? [22]
[22] Musa akaashiria sifa katika sifa ovu kabisa za Firauni, nayo ni kuwa kawafanya watumwa Wana wa Israili, na akiwauwa watoto wao wanaume. Na akakataa kukuita kule kulelewa kwake katika jumba la Firauni kuwa ni neema, kwani yaliyo sabibisha hayo ni yale aliyo kwisha yataja, ndio yeye alitupwa mtoni aokoke asiuliwe. Akaishia kwenye jumba la Firauni. Na lau kuwa si hivyo basi angeli lelewa na wazazi wake.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na kwani huko kulelewa nyumbani kwako unakuona ni neema kutoka kwako juu yangu, na hali wewe umewafanya Wana wa Isrãîl ni watumwa, unawachinja wana wao wa kiume na unawaachilia wanawake wao ili watumwe na wadharauliwe?»
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net