Ash-Shu'araa 26:209
الشعراءذِكْرَىٰ وَمَا كُنَّا ظَـٰلِمِينَ
Kuwa ni ukumbusho. Wala Sisi hatukuwa wenye kudhulumu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Kuwa ni ukumbusho. Wala Sisi hatukuwa wenye kudhulumu. [209]
[209] Wakumbuke na wazingatie. Wala si shani yetu kudhulumu hata tuuadhibu umma kabla ya kuwaletea Mtume.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Ili wawe ni ukumbusho kwao na uzindushi wa yale yenye uokovu kwao. Na hatukuwa ni wenye kudhulumu kwani hatukuwaadhibu watu kabla ya kuwapelekea Mtume.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net