Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 26 · Aya ya 194

Ash-Shu'araa 26:194

الشعراء

عَلَىٰ قَلْبِكَ لِتَكُونَ مِنَ ٱلْمُنذِرِينَ

Maana

Juu ya moyo wako, ili uwe katika Waonyaji.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Juu ya moyo wako, ili uwe katika Waonyaji,. [194]

[194] Juu ya moyo wako ulio tulia kuihifadhi na kuifahamu, na idhibitike katika moyo wako iwe madhubuti isisahaulike, ili upate kuwaonya wakhalifu kwa adhabu ziliomo ndani yake.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Akakusomea mpaka ukaikusanya moyoni mwako, kwa kuihifadhi na kuielewa, upate kuwa ni mmoja wa wajumbe wa Allah Mtukufu wenye kuwafanya watu wao waogope mateso ya Allah Mtukufu, upate kuwaonya, kwa Teremsho hili, binadamu na majini wote.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Ash-Shu'araa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net