Ash-Shu'araa 26:192
الشعراءوَإِنَّهُۥ لَتَنزِيلُ رَبِّ ٱلْعَـٰلَمِينَ
Na bila ya shaka hii ni Uteremsho wa Mola Mlezi wa walimwengu wote.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na bila ya shaka hii ni Uteremsho wa Mola Mlezi wa walimwengu wote. [192]
[192] Na hakika hii Qur'ani iliyo tajwa ndani yake visa vya kweli imeteremshwa kutoka kwa Mwenye kuumba walimwengu wote, Mwenye kumiliki mambo yao, na Mlezi wao. Basi khabari zake ni za kweli. Na hukumu yake inatimizwa mpaka Siku ya Kiyama.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na kwa hakika, hii Qur’ani ambayo ndani yake zimetajwa habari hizi za kweli imeteremshwa na Muumba wa viumbe na Mmiliki wa mambo yote.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net