Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 26 · Aya ya 187

Ash-Shu'araa 26:187

الشعراء

فَأَسْقِطْ عَلَيْنَا كِسَفًا مِّنَ ٱلسَّمَآءِ إِن كُنتَ مِنَ ٱلصَّـٰدِقِينَ

Maana

Hebu tuangushie vipande kutoka mbinguni ikiwa wewe ni miongoni mwa wakweli.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Hebu tuangushie vipande kutoka mbinguni ikiwa wewe ni miongoni mwa wasemao kweli. [187]

[187] Basi hebu tuangushie vipande vya adhabu kutoka mbinguni ikiwa ni katika wasemao kweli kwa huu ujumbe wako! Na chini ya shauri hii kwa hakika pana kila namna ya ubishi.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Iwapo wewe ni mkweli katika madai yako ya utume, basi muombe Allah Mtukufu Atuangushie vipande vya adhabu kutoka mbinguni vitumalize.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Ash-Shu'araa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net