Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 26 · Aya ya 183

Ash-Shu'araa 26:183

الشعراء

وَلَا تَبْخَسُوا۟ ٱلنَّاسَ أَشْيَآءَهُمْ وَلَا تَعْثَوْا۟ فِى ٱلْأَرْضِ مُفْسِدِينَ

Maana

Wala msiwapunje watu vitu vyao, wala msifanye jeuri katika ardhi kwa kufanya uharibifu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Wala msiwapunje watu vitu vyao, wala msifanye jeuri kwa ufisadi. [183]

[183] Wala msiwapunguzie watu haki zao, wala msipite katika nchi mkifisidi kwa kuuwa, na uharamia, na kufanya madhambi, na kufuata pumbao.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na msiwapunje watu chochote katika haki zao kwenye vipimo au mizani au vinginevyo, na msizidishe uharibifu katika ardhi kwa kufanya ushirikina. kuua, kunyang’anya, kuwatisha watu na kutekeleza vitendo vya uasi.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Ash-Shu'araa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net