Ash-Shu'araa 26:133
الشعراءأَمَدَّكُم بِأَنْعَـٰمٍ وَبَنِينَ
Aliwapa wanyama wa kufuga na wana.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Amekupeni wanyama wa kufuga na wana. [133]
[133] Kama alivyo kupeni mifugo kama ngamia, na ng'ombe, na kondoo, na mbuzi, na wana wenye nguvu, wakukulindieni mifugo yenu, na kukusaidieni katika shida za maisha.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Amewapa wanyama hawa: ngamia ng’ombe, mbuzi na kondoo, na Amewapa watoto.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net