Ash-Shu'araa 26:130
الشعراءوَإِذَا بَطَشْتُم بَطَشْتُمْ جَبَّارِينَ
Na mnapotumia nguvu, mnatumia nguvu kwa ujabari.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na mnapo tumia nguvu mnatumia nguvu kwa ujabari. [130]
[130] Na mnapo ingia kutesa, mnapita kiasi katika uasi na uvamizi wa jeuri, mnauwa, na mnapiga kwa chuki bila ya huruma.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na mnapomshika mtu kwa nguvu na kuweza kumuua au kumpiga, basi mnalifanya hilo kwa kutendesha nguvu hali ya kufanya maonevu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net