Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 26 · Aya ya 128

Ash-Shu'araa 26:128

الشعراء

أَتَبْنُونَ بِكُلِّ رِيعٍ ءَايَةً تَعْبَثُونَ

Maana

Je, mnajenga juu ya kila mnyanyuko kumbusho la kufanyia upuuzi?

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Je! Mnajenga juu ya kila mnyanyuko kumbusho la kufanyia upuuzi? [128]

[128] Je! Mnasimamisha juu ya kila pahala palipo nyanyuka katika nchi jengo refu kwa ajili ya kujifakhirisha, na mnakutana humo kwa mambo ya upuuzi na fisadi? Mwenyezi Mungu Subhanahu anataka kwa haya kuwazindua watende yatakayo wanufaisha, na anawatahayarisha kwa kuacha kwao Imani na vitendo vyema.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Je mnajenga kila mahali palipoinuka jengo refu mkawa mnatazama kutoka hapo na mnawacheza shere wapita njia? Huo ni upuuzi na upitaji kiasi, na hauwaletei nyinyi faida yoyote katika dini au katika dunia.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Ash-Shu'araa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net