Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 26 · Aya ya 12

Ash-Shu'araa 26:12

الشعراء

قَالَ رَبِّ إِنِّىٓ أَخَافُ أَن يُكَذِّبُونِ

Maana

Akasema: Mola wangu Mlezi, hakika mimi ninachelea kwamba watanikadhibisha.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Akasema: Hakika mimi nachelea wasinikanushe. [12]

[12] Musa akasema: Ewe Mola wangu Mlezi! Mimi nina khofu wasije kuukataa ujumbe wangu kwa kiburi na inda.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Mûsã akasema, «Mola wangu! Mimi ninaogopa wasije wakanikanusha juu ya utume».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Ash-Shu'araa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net