Ash-Shu'araa 26:114
الشعراءوَمَآ أَنَا۠ بِطَارِدِ ٱلْمُؤْمِنِينَ
Wala mimi si wa kuwafukuza Waumini.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Wala mimi si wa kuwafukuza Waumini. [114]
[114] Wala mimi siye wa kuwafukuza watu wanao uamini wito wangu vyovyote itavyo kuwa hali yao ya ufakiri au utajiri, kwa sababu ati ya kukubalieni nyinyi kwa mtakalo ili ndio mpate kuniamini.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na mimi si mwenye kuwafukuza wale wanaouamini ulinganizi wangu, kwa namna yoyote itakavyokuwa hali yao, kwa kufuata matakwa yenu, ili mniamini.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net