Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 25 · Aya ya 77

Al-Furqaan 25:77

الفرقان

قُلْ مَا يَعْبَؤُا۟ بِكُمْ رَبِّى لَوْلَا دُعَآؤُكُمْ ۖ فَقَدْ كَذَّبْتُمْ فَسَوْفَ يَكُونُ لِزَامًۢا

Maana

Sema: Mola wangu Mlezi asingewajali lau kuwa si kuomba kwenu. Lakini nyinyi mmemkadhibisha. Basi adhabu lazima iwe.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Sema: Mola wangu Mlezi asinge kujalini lau kuwa si kuomba kwenu. Lakini nyinyi mmemkadhibisha. Basi adhabu lazima iwe. [77]

[77] Ewe Mtume! Waambie watu: Mwenyezi Mungu hakutakini nyinyi ila mumuabudu Yeye, na mumwombe Yeye katika mambo yenu, wala msimwombe yeyote mwenginewe. Na kwa hayo ndio kakuumbeni. Lakini makafiri katika nyinyi wameyakanusha waliyo kuja nayo Mitume. Basi adhabu yao itawaganda hao, wala hapana wa kuwaokoa nayo.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Allah Mtukufu Anatoa habari kuwa Yeye hawajali watu wala hashughuliki nao lau si wao kumuomba Yeye maombi ya ibada na maombi ya kutaka msaada, Hakika yenu nyinyi, enyi makafiri, mmekanusha, na ukanushaji wenu utapelekea mpate adhabu yenye kuwa na nyinyi, kama vile mwenye kudai anavyokuwa na mdaiwa wake, na Atawaangamiza duniani na Akhera.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Furqaan

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net