Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 25 · Aya ya 7

Al-Furqaan 25:7

الفرقان

وَقَالُوا۟ مَالِ هَـٰذَا ٱلرَّسُولِ يَأْكُلُ ٱلطَّعَامَ وَيَمْشِى فِى ٱلْأَسْوَاقِ ۙ لَوْلَآ أُنزِلَ إِلَيْهِ مَلَكٌ فَيَكُونَ مَعَهُۥ نَذِيرًا

Maana

Na wakasema: Ana nini Mtume huyu? Anakula chakula, na anatembea masokoni! Mbona hakuteremshiwa Malaika akawa mwonyaji pamoja naye?

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na wakasema: Ana nini Mtume huyu? Anakula chakula, na anatembea masokoni! Mbona hakuteremshiwa Malaika akawa mwonyaji pamoja naye? [7]

[7] Wakamkejeli Muhammad, wakasema: Kitu gani kinacho mtengua huyu anaye dai kuwa ni Mtume, hata anakula chakula kama tulavyo sisi, na anazururuka masokoni kutafuta maisha kama watu wengine? Angeli kuwa ni Mtume Mwenyezi Mungu angeli mtosheleza kwa hayo, na yeye angeli mwomba Mola wake Mlezi amteremshie Malaika kutoka mbinguni amsaidie katika uwonyaji na kufikisha Ujumbe, na amsadikishe katika wito wake, tupate sisi kumuamini.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na walisema washirikina, «Ana nini huyu anayedai kwamba yeye ni Mtume wa Allah Mtukufu (wakimkusudia Muhammad, rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie), anakula chakula kama sisi na anaenda sokoni kutafuta riziki? Basi si angemtuma Malaika awe naye ashuhudilie ukweli wake?»

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Furqaan

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net