Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 25 · Aya ya 64

Al-Furqaan 25:64

الفرقان

وَٱلَّذِينَ يَبِيتُونَ لِرَبِّهِمْ سُجَّدًا وَقِيَـٰمًا

Maana

Na wale wanaokesha kwa ajili ya Mola wao Mlezi kwa kusujudu na kusimama.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na wale wanao kesha kwa ajili ya Mola wao Mlezi kwa kusujudu na kusimama. [64]

[64] Na wale ambao wanakesha katika ibada na Sala, wakimdhukuru Mwenyezi Mungu kwa wingi.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na ambao wanaswali usiku kwa wingi wakimtakasia Mola wao, wakiwa ndani ya Swala na wakijidhalilisha Kwake kwa kusujudu na kusimama.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Furqaan

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net