Al-Furqaan 25:62
الفرقانوَهُوَ ٱلَّذِى جَعَلَ ٱلَّيْلَ وَٱلنَّهَارَ خِلْفَةً لِّمَنْ أَرَادَ أَن يَذَّكَّرَ أَوْ أَرَادَ شُكُورًا
Naye ndiye aliyefanya usiku na mchana kufuatana kwa nafuu ya yule anayetaka kukumbuka, au anayetaka kushukuru.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Naye ndiye aliye fanya usiku na mchana kufuatana kwa nafuu ya anaye taka kukumbuka, au anaye taka kushukuru. [62]
[62] Mwingi wa Rehema ndiye aliye ufanya usiku na mchana kufuatana, mmoja nyuma ya mwenzie. Na tumeyapanga haya ili mwenye kutaka akumbuke mpango huu, na ajue hikima ya Mwenyezi Mungu na uweza wake; au apate kushukuru kwa neema hii njema.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na Yeye Ndiye Aliyefanya usiku na mchana vipishane, kimoja baada ya kingine, kwa anayetaka kuzingatia hilo kwa kumuamini Allah Mtukufu, Mpelekeshaji mambo na Muumbaji au anayetaka kumshukuru Allah Mtukufu, Aliyetukuka, kwa neema Zake na mema Yake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net