Al-Furqaan 25:46
الفرقانثُمَّ قَبَضْنَـٰهُ إِلَيْنَا قَبْضًا يَسِيرًا
Kisha tunakivutia kwetu kidogo kidogo.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Kisha tunakivutia kwetu kidogo kidogo. [46]
[46] Na kukiondoa kwetu kivuli ni kwa utaratibu, kwa kipimo. Hakukuwa kwa mara moja. Na katika hayo yapo manufaa kwa watu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Kisha kivuli kinapotea kidogo kidogo, kila kunapoongezeka kupaa juu kwa jua ndipo kunapoongezeka kupungua kwake. Hilo ni miongoni mwa dalili za uwezo wa Allah Mtukufu, ukubwa Wake, na kwamba Yeye Peke Yake Ndiye Anayestahiki kuabudiwa, si mwengine.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net