Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 25 · Aya ya 34

Al-Furqaan 25:34

الفرقان

ٱلَّذِينَ يُحْشَرُونَ عَلَىٰ وُجُوهِهِمْ إِلَىٰ جَهَنَّمَ أُو۟لَـٰٓئِكَ شَرٌّ مَّكَانًا وَأَضَلُّ سَبِيلًا

Maana

Wale ambao watakusanywa kwa nyuso zao hadi katika Jahannamu, hao watakuwa na mahali pabaya mno, nao ndio wenye kuipotea zaidi njia.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Wale ambao watakao kusanywa na kubururwa kifudifudi mpaka kwenye Jahannamu, hao watakuwa na mahali pabaya, ndio wenye kuipotea sana njia. [34]

[34] Na walio ukataa Ujumbe wako watabururwa kupelekwa Motoni kifudifudi na madhalili. Hao ndio watu wa chini kabisa kwa cheo, na ndio walio zama mno katika upotovu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hao makafiri ndio watakaoburutwa kwa nyuso zao hadi kwenye Moto wa Jahanamu. Hao ndio wenye mashukio mabaya kabisa miongoni mwa watu, na ndio walioko mbali kabisa na njia ya haki.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Furqaan

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net