Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 25 · Aya ya 3

Al-Furqaan 25:3

الفرقان

وَٱتَّخَذُوا۟ مِن دُونِهِۦٓ ءَالِهَةً لَّا يَخْلُقُونَ شَيْـًٔا وَهُمْ يُخْلَقُونَ وَلَا يَمْلِكُونَ لِأَنفُسِهِمْ ضَرًّا وَلَا نَفْعًا وَلَا يَمْلِكُونَ مَوْتًا وَلَا حَيَوٰةً وَلَا نُشُورًا

Maana

Na wamechukua badala yake miungu ambayo haiumbi chochote, bali hiyo inaumbwa, haijimilikii nafsi zao madhara wala manufaa, wala haimiliki mauti, wala uhai, wala kufufuka.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na wamechukua badala yake miungu ambayo haiumbi chochote, bali hiyo inaumbwa, haijimilikii nafsi zao madhara wala manufaa, wala haimiliki mauti, wala uhai, wala kufufuka. [3]

[3] Na juu ya yote hayo makafiri wakaacha kumuabudu Yeye, wakenda kuchukua miungu mingine kuiabudu badala ya Mwenyezi Mungu, katika masanamu, na nyota, na watu. Na hao hawanalo waliwezalo kuliumba, bali wao ni viumbe vya Mwenyezi Mungu. Wala hawawezi kujikinga nafsi zao na madhara, wala kujiletea kheri. Wala hawawezi kumfisha yeyote wala kumhuisha, wala kuwafufua maiti kutoka makaburini kwao. Na kila asiye miliki lolote katika hayo basi hastahiki kuabudiwa. Na mjinga wa kutupwa anaye waabudu. Mwenye kustahiki kuabudiwa ni yule Mwenye kumiliki haya yote.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na washirikina wa kiarabu walitengeneza waungu, wasiokuwa Allah Mtukufu. Waungu hao hawawezi kuumba chochote, na Allah Mtukufu Ndiye Aliyewaumba wao na wenye kuwaabudu, wala hawana uwezo wa kuzuia madhara wala kujiletea manufaa, wala hawawezi kukifisha kilicho hai wala kukihuisha kilichokufa au kumfufua yoyote, miongoni mwa wafu, akiwa hai kutoka kaburini mwake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Furqaan

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net