An-Noor 24:6
النوروَٱلَّذِينَ يَرْمُونَ أَزْوَٰجَهُمْ وَلَمْ يَكُن لَّهُمْ شُهَدَآءُ إِلَّآ أَنفُسُهُمْ فَشَهَـٰدَةُ أَحَدِهِمْ أَرْبَعُ شَهَـٰدَٰتٍۭ بِٱللَّهِ ۙ إِنَّهُۥ لَمِنَ ٱلصَّـٰدِقِينَ
Na wale wanaowasingizia wake zao uzinzi na hawana mashahidi ila nafsi zao, basi ushahidi wa mmoja wao utakuwa kushuhudilia mara nne kwa kiapo cha Mwenyezi Mungu, ya kwamba hakika yeye ni katika wasemao ukweli.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na wale wanao wasingizia wake zao na hawana mashahidi ila nafsi zao, basi ushahidi wa mmoja wao utakuwa kushuhudilia mara nne kwa kiapo cha Mwenyezi Mungu ya kwamba hakika yeye ni katika wasema kweli. [6]
[6] Na hao wanao watuhumu wake zao kuwa wamezini na hawana mashahidi wanao takikana kushuhudia ukweli wa tuhuma yao, basi anatakikana mmoja wa hao kama anataka isimpate adhabu, ashuhudie kwa Mwenyezi Mungu mara nne kuwa yeye ni mkweli katika hiyo tuhuma yake.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na wale wanaowatuhumu wake zao kwa uzinifu, na wakawa hawana mashahidi wa kutilia nguvu tuhuma yao isipokuwa wao wenyewe, basi ni juu ya mmoja wao hao wenye kutuhumu, atoe ushahidi mbele ya kadhi mara nne kwa kusema, «Ninashuhudia kwa jina la Allah Mtukufu kwamba mimi ni mkweli katika lile la uzinifu ambalo nimemtuhumu mke wangu kwalo».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net