An-Noor 24:46
النورلَّقَدْ أَنزَلْنَآ ءَايَـٰتٍ مُّبَيِّنَـٰتٍ ۚ وَٱللَّهُ يَهْدِى مَن يَشَآءُ إِلَىٰ صِرَٰطٍ مُّسْتَقِيمٍ
Kwa yakini tumeteremsha Ishara zinazobainisha. Na Mwenyezi Mungu humwongoa amtakaye kwenye Njia iliyonyooka.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Kwa yakini tumeteremsha Ishara zinazo bainisha. Na Mwenyezi Mungu hummwongoa amtakaye kwenye Njia Iliyo Nyooka. [46]
[46] Na hakika Sisi tumeteremsha kwa wahyi Aya zilizo wazi za kubainisha hukumu na mawaidha, na zinazo piga mifano. Na Mwenyezi Mungu humwezesha kwenye kheri ampendaye katika waja wake ambao wapo tayari kuziangalia na kufaidika nazo.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na kwa hakika tumeteremsha katika Qur’ani vitambulisho vilivyo waziwazi vyenye kuongoza kwenye haki. Na Allah Mtukufu Anamuongoza na kumuelekeza Anayemtaka katika waja wake kwenye njia iliyolingana sawa, nayo ni Uislamu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net