An-Noor 24:41
النورأَلَمْ تَرَ أَنَّ ٱللَّهَ يُسَبِّحُ لَهُۥ مَن فِى ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضِ وَٱلطَّيْرُ صَـٰٓفَّـٰتٍ ۖ كُلٌّ قَدْ عَلِمَ صَلَاتَهُۥ وَتَسْبِيحَهُۥ ۗ وَٱللَّهُ عَلِيمٌۢ بِمَا يَفْعَلُونَ
Je, huoni kwamba Mwenyezi Mungu vinamtakasa vilivyo katika mbingu na ardhi, na ndege wakikunjua mbawa zao? Kila mmoja amekwisha jua Swala yake na namna ya kumtakasa kwake. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuyajua wayatendayo.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Je! Huoni kwamba Mwenyezi Mungu vinamtakasa vilivyomo katika mbingu na ardhi, na ndege wakikunjua mbawa zao? Kila mmoja amekwisha jua Sala yake na namna ya kumtakasa kwake. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuyajua wayatendayo. [41]
[41] Ewe Nabii! Hujui kwa yakini kwamba kwa Mwenyezi Mungu hunyenyekea kila kiliomo mbinguni na duniani? Na wanamnyenyekea ndege vile vile, nao wamekunjua mbawa zao? Basi viumbe vyote hivi vinanyenyekea amri ya Mwenyezi Mungu na mipango yake. Vinamtakasa na washirika na kila lisio na laiki naye. Na kila kimojawapo kinajua kwa kujaaliwa na Mwenyezi Mungu yaliyo kiwajibikia katika unyenyekevu na kutakasa na kutimiza wadhifa wa maisha. Na Mwenyezi Mungu nyuma yao anajua kwa utimilivu wa kujua Swala ya kila mwenye kusali, na kusabihi kwa mwenye kusabihi, na yote wayafanyayo waja. Basi huwaje makafiri wakawa hawaamini?
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Kwani hukujua, ewe Mtume, kwamba Allah Mtukufu vinamtakasa Yeye viumbe vilivyoko mbinguni na ardhini. Na ndege wamezikunjua mbawa zao huko juu angani wanamtakasa Mola wao? Kila kiumbe, Allah Mtukufu Amemfundisha namna ya kumswalia na ya kumtakasa. Na Yeye, kutakasika na sifa za upungufu ni Kwake, Anayaona anayoyafanya kila mwenye kuabudu na kutakasa, hakuna chochote kinachofichika Kwake kuhusu hayo, na Atawalipa kwa hayo.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net