Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 23 · Aya ya 91

Al-Muminoon 23:91

المؤمنون

مَا ٱتَّخَذَ ٱللَّهُ مِن وَلَدٍ وَمَا كَانَ مَعَهُۥ مِنْ إِلَـٰهٍ ۚ إِذًا لَّذَهَبَ كُلُّ إِلَـٰهٍۭ بِمَا خَلَقَ وَلَعَلَا بَعْضُهُمْ عَلَىٰ بَعْضٍ ۚ سُبْحَـٰنَ ٱللَّهِ عَمَّا يَصِفُونَ

Maana

Mwenyezi Mungu hana mwana yeyote, wala hanaye mungu mwingine. Ingekuwa hivyo basi kila mungu angelichukua alivyoumba, na baadhi yao wangeliwashinda wengine. Mwenyezi Mungu ameepukana na sifa wanazomsifu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Mwenyezi Mungu hana mwana yeyote, wala hanaye mungu mwengine. Inge kuwa hivyo basi kila mungu angeli chukua alivyo umba, na baadhi yao wangeli washinda wengine. Mwenyezi Mungu ameepukana na sifa wanazo msifu. [91]

[91] Mwenyezi Mungu hakumchukua yeyote kuwa ni mwanawe. Yeye ametakasikia na hayo. Wala hana mshirika. Angeli kuwa na mshirika basi kila mmoja wao angejipa madaraka ya pekee kwa alivyo viumba, na vikawa ndio milki yake, na wangeli gombana wenyewe kwa wenyewe kama wanavyo onekana wafalme wanavyo fanya. Na ulimwengu ungeli fisidika kwa mizozano hiyo. Basi Mwenyezi Mungu ametakasika na hayo wayasemayo washirikina yanayo kwenda kinyume na Haki.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Allah Mtukufu Hakujifanyia mtoto, na hakukuwa pamoja na Yeye muabudiwa mwingine, kwani kama kungekua huko kuna waabudiwa zaidi ya mmoja pamoja na Yeye, basi kila muabudiwa angejitenga na alivyoviumba na kungekua na ushindani kati yao kama ilivyo kwa watawala wa ulimwenguni. Hapo mpangilio wa ulimwengu ungeharibika. Ametakasika Allah Mtukufu Aliyetukuka na sifa wanazompa za kuwa Yeye ana mshirika au mtoto.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Muminoon

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net