Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 23 · Aya ya 70

Al-Muminoon 23:70

المؤمنون

أَمْ يَقُولُونَ بِهِۦ جِنَّةٌۢ ۚ بَلْ جَآءَهُم بِٱلْحَقِّ وَأَكْثَرُهُمْ لِلْحَقِّ كَـٰرِهُونَ

Maana

Au wanasema: Ana wazimu? Bali amewajia kwa Haki, na wengi wao wanaichukia Haki.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Au wanasema: Ana wazimu? Bali amewajia kwa Haki, na wengi wao wanaichukia Haki. [70]

[70] Au wanasema kuwa huyu ni mwendawazimu? Hasha! Huyu hakika kawaletea Dini ya Haki, na wengi wao wanaichukia haki, kwani hiyo ni kinyume na matamanio yao na mapenzi yao, basi kwa hivyo hawamuamini.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Au wanamdhania kuwa ni mwendawazimu? Kwa hakika wamedanganya. Ukweli ni kuwa amewajia na Qur’ani, na upwekeshaji Allah Mtukufu, na dini ya kweli. Na wengi wao wanaichukia haki kwa uhasidi na uadui.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Muminoon

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net