Al-Muminoon 23:60
المؤمنونوَٱلَّذِينَ يُؤْتُونَ مَآ ءَاتَوا۟ وَّقُلُوبُهُمْ وَجِلَةٌ أَنَّهُمْ إِلَىٰ رَبِّهِمْ رَٰجِعُونَ
Na wale ambao wanatoa kile walichopewa, na hali nyoyo zao zinaogopa kwa kuwa watarejea kwa Mola wao Mlezi.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na wale ambao wanatoa walicho pewa, na hali nyoyo zao zinagopa kwa kuwa watarejea kwa Mola wao Mlezi, [60]
[60] Na wale ambao wanatoa katika vile anavyo waruzuku Mwenyezi Mungu, na wanafanya a'mali yao na hali wao wana khofu wasifanye taksiri, kwa sababu bila ya shaka wao ni wenye kurejea kwa Mwenyezi Mungu kwa kufufuliwa na watahisabiwa,
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na wale wanaojibidiisha kufanya matendo ya kheri na wema, mioyo yao ina hofu ya kuogopa yasikubaliwe matendo yao na yasiwaokoe na adhabu ya Mola wao warejeapo Kwake kwa kuhesabiwa.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net