Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 23 · Aya ya 56

Al-Muminoon 23:56

المؤمنون

نُسَارِعُ لَهُمْ فِى ٱلْخَيْرَٰتِ ۚ بَل لَّا يَشْعُرُونَ

Maana

Ndiyo tunawaharakishia heri? Lakini wenyewe hawatambui.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Ndio tunawahimizia kheri? Lakini wenyewe hawatambui. [56]

[56] Ndio basi Sisi tumekuwa radhi nao, na kheri zikawamiminikia mbio mbio na kwa wingi? Hao ni kama wanyama, hawatambui, kwa kuwa hawazitumii akili zao. Mimi si radhi nao. Na hizi neema ni kuwapururia tu, kuwapa muda.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hakika tunawaharakishia haya mazuri kwa kuwatahini na kwa kuwavuta kidogo kidogo, lakini wao hawalihisi hilo.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Muminoon

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net