Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 23 · Aya ya 50

Al-Muminoon 23:50

المؤمنون

وَجَعَلْنَا ٱبْنَ مَرْيَمَ وَأُمَّهُۥٓ ءَايَةً وَءَاوَيْنَـٰهُمَآ إِلَىٰ رَبْوَةٍ ذَاتِ قَرَارٍ وَمَعِينٍ

Maana

Na tukamfanya mwana wa Mariamu na mama yake kuwa ni Ishara, na tukawapa makimbilio kwenda mahali palipoinuka penye utulivu na chemchemi za maji.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na tukamfanya mwana wa Mariamu na mama yake kuwa ni Ishara, na tukawapa makimbilio kwenda mahali palipo inuka penye utulivu na chemchem za maji. [50]

[50] Na tumemjaalia Isa bin Maryamu na mama yake, kwa vile kuchukua mimba bila ya kuingiliwa na mtu, na kuzaliwa yeye Isa bila ya baba, kuwa dalili ya kukata ya uwezo wetu wenye kushinda. Na tukamweka Maryamu pahala pa kukaa penye ardhi iliyo nyanyuka na kukunjuka panapo faa kukaa, na pana maji mengi. Na hayo ndiyo yanayo wezesha maisha ya starehe.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na tulimjaalia ‘Ǐsâ mwana wa Maryam na mama yake kuwa ni alama yenye kuonesha uwezo wetu, kwani tulimuumba bila ya baba, na tulimfanyia makao kwenye ardhi iliyopo mahali pa juu palipolingana ili apate utulivu juu yake, penye urutuba na maji yapitayo yanayoonekana waziwazi kwa macho.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Muminoon

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net