Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 23 · Aya ya 13

Al-Muminoon 23:13

المؤمنون

ثُمَّ جَعَلْنَـٰهُ نُطْفَةً فِى قَرَارٍ مَّكِينٍ

Maana

Kisha tukamfanya kuwa tone la mbegu ya uzazi katika mahali patulivu palipo madhubuti.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Kisha tukamjaalia awe tone ya mbegu ya uzazi katika kalio madhubuti. [13]

[13] Kisha tukaumba vizazi vyake, navyo ni kuwa tulimfanya mtu kwanza tone ya mbegu ya uzazi - yaani maji yenye kila sifa ya uhai wa mwanzo. Tukaiweka kwenye tumbo la uzazi, napo ni pahala pa utulivu palipo lindwa.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Kisha tukawaumba watoto wake wakiwa ni wenye kuzaana kutokana na tone la maji: nalo ni manii ya wanaume, yanatoka kwenye migongo yao na yanatulia ndani ya vizazi vya wanawake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Muminoon

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net