Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 23 · Aya ya 108

Al-Muminoon 23:108

المؤمنون

قَالَ ٱخْسَـُٔوا۟ فِيهَا وَلَا تُكَلِّمُونِ

Maana

Atasema Mwenyezi Mungu: Tokomeeni humo, wala msinisemeshe.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Atasema Mwenyezi Mungu: Tokomeeni humo, wala msinisemeze. [108]

[108] Na Mwenyezi Mungu atawaambia kwa kuwadharau na kuwabeza: Kaeni humo kwa madhila na unyonge, wala msiseme nami kabisa!

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Allah Mtukufu, Aliyeshinda na kutukuka, Atawaambia, «Kaeni Motoni mkiwa wanyonge wala msiseme na mimi.» Hapo yatakatika maombi yao na matumaini yao.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Muminoon

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net