Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 23 · Aya ya 106

Al-Muminoon 23:106

المؤمنون

قَالُوا۟ رَبَّنَا غَلَبَتْ عَلَيْنَا شِقْوَتُنَا وَكُنَّا قَوْمًا ضَآلِّينَ

Maana

Watasema: Mola wetu Mlezi! Tulizidiwa na uovu wetu na tukawa watu tuliopotea.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Mola wetu Mlezi! Tulizidiwa na uovu wetu na tukawa watu tulio potea. [106]

[106] Watasema nao wanakiri makosa yao : Ewe Mola wetu Mlezi! Maasi yetu yalikuwa mengi, ndio yakatupatia mashaka, na tukawa wenye kupotea tukaiacha njia ya sawa.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Watakubali kuwa Mitume wao waliwapelekea ujumbe na wakawaonya, watasema Siku ya Kiyama, «Mola wetu! Raha zetu, na pia matamanio yetu yalikadiriwa kwetu kwenye ujuzi wako uliotangulia, zilitutawala na kwa hivyo tukawa, katika matendo yetu, ni wenye kupotea na kuwa kando ya njia ya uongofu».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Muminoon

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net