Al-Muminoon 23:101
المؤمنونفَإِذَا نُفِخَ فِى ٱلصُّورِ فَلَآ أَنسَابَ بَيْنَهُمْ يَوْمَئِذٍ وَلَا يَتَسَآءَلُونَ
Basi litakapopulizwa baragumu, hapo hautakuwapo ujamaa baina yao siku hiyo, wala hawataulizana.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Basi litapo pulizwa baragumu hapo hautakuwapo ujamaa baina yao siku hiyo, wala hawataulizana. [101]
[101] Ukifika wakati wa kufufuliwa tutawafufua kutoka makaburini kwao. Na hayo ni kwa mfano wa kupulizwa tarumbeta watafufuka nao wamefarikiana. Hapana mtu utaomfaa ujamaa wake na fulani. (Ujamaa Kiswahili maana yake makhusiano ya nasaba, sio usoshalisti.) Wala hapana mtu atae muomba mtu kitu cha kumfaa. Kwani kila mmoja wao siku hiyo atakuwa kashughulika na lake.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Basi Siku ya Kiyama itakapokuwa, na Malaika anayehusika akapuliza kwenye baragumu, na watu wakafufuliwa kutoka makaburini mwao, hapo hakuna kujigamba kwa nasaba kama walivyokuwa wakijigamba nazo duniani, wala hapana yoyote atakayemuuliza yoyote.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net