Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 22 · Aya ya 77

Al-Hajj 22:77

الحج

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ ٱرْكَعُوا۟ وَٱسْجُدُوا۟ وَٱعْبُدُوا۟ رَبَّكُمْ وَٱفْعَلُوا۟ ٱلْخَيْرَ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ ۩

Maana

Enyi mlioamini! Rukuuni na sujuduni, na muabuduni Mola wenu Mlezi, na tendeni mema, ili mfanikiwe.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Enyi mlio amini! Rukuuni na msujudu, na muabuduni Mola wenu Mlezi, na tendeni mema, ili mfanikiwe. [77]

[77] Enyi mlio amini! Msishughulikie upotovu wa makafiri. Nyinyi endeleeni na kutimiza Swala zenu kwa ukamilifu kwa kurukuu na kusujudu. Na muabuduni Mola wenu Mlezi aliye kuumbeni na akakuruzukuni. Wala msimshirikishe naye na yeyote. Na tendeni kila lenye kheri na manufaa, ili mpate kuwa watu wema, walio bahatika katika Akhera yenu na dunia yenu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Enyi mliomuamini Allah Mtukufu na Mtume Wake Muhammad, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie), rukuuni na sujuduni katika Swala zenu na muabuduni Mola wenu, Peke Yake, Asiye na mshirika, na fanyeni wema ili mufuzu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Hajj

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net