Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 22 · Aya ya 42

Al-Hajj 22:42

الحج

وَإِن يُكَذِّبُوكَ فَقَدْ كَذَّبَتْ قَبْلَهُمْ قَوْمُ نُوحٍ وَعَادٌ وَثَمُودُ

Maana

Na wakikukanusha, basi walikwishakanusha kabla yao watu wa Nuhu, na kina 'Aad na kina Thamud.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na wakikukanusha basi walikwisha kanusha kabla yao watu wa Nuhu, na kina A'ad na kina Thamud, [42]

[42] Ewe Nabii! Ukiwa unapata makanusho, kuambiwa mwongo, na maudhi kutokana na watu wako, basi usisikitike. Zingatia taarikh kwa yaliyo wapata Mitume wa kabla yako, utaona kwamba wewe si Mtume wa kwanza aliye kanushwa na kuudhiwa na watu wake. Kwani kabla ya hawa walio kukanusha wewe, kaumu Nuhu walimkadhibisha Mtume wao Nuhu, na kaumu ya A'ad walimkadhibisha Mtume wao Huud, na kina Thamud walimkanusha Mtume wao Swaleh.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na wakikukanusha watu wako, ewe Mtume, basi wamewatangulia wao katika kukanusha Mitume wao watu wa Nûḥ, ‛Ãd, Thamûd.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Hajj

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net