Al-Anbiyaa 21:69
الأنبياءقُلْنَا يَـٰنَارُ كُونِى بَرْدًا وَسَلَـٰمًا عَلَىٰٓ إِبْرَٰهِيمَ
Sisi tukasema: Ewe moto! Kuwa baridi na salama kwa Ibrahim!
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Sisi tukasema: Ewe moto! Kuwa baridi na salama kwa Ibrahim! [69]
[69] Sisi tukaufanya moto ule uwe baridi na salama, hauna madhara yoyote, kwa Ibrahim.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Allah Mtukufu Akamsaidia Mtume Wake na Akauambia moto, «Kuwa baridi na salama kwa Ibrãhîm!» Hivyo basi asipatwe na udhia wala asifikiwe na jambo la kuchukiza.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net