Al-Anbiyaa 21:60
الأنبياءقَالُوا۟ سَمِعْنَا فَتًى يَذْكُرُهُمْ يُقَالُ لَهُۥٓ إِبْرَٰهِيمُ
Wakasema: Tumemsikia kijana mmoja akiwataja. Anaitwa Ibrahim.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Wakasema: Tumemsikia kijana mmoja akiwataja. Anaitwa Ibrahim. [60]
[60] Wakasema baadhi yao: Tumemsikia kijana mmoja akiitaja kwa kuisubu (kuitukana) ; naye anaitwa Ibrahim.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hapo wale waliomsikia Ibrãhîm akiapa kwamba atawachimba masanamu wao wakasema, «Tulimsikia kijana akiwataja kwa ubaya, anaitwa Ibrãhîm».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net