Al-Anbiyaa 21:58
الأنبياءفَجَعَلَهُمْ جُذَٰذًا إِلَّا كَبِيرًا لَّهُمْ لَعَلَّهُمْ إِلَيْهِ يَرْجِعُونَ
Basi akayavunja vipande vipande, ila kubwa lao, ili wao walirudie.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Basi akayavunja vipande vipande, ila kubwa lao, ili wao walirudie. [58]
[58] Baada ya kwisha ondoka wale watu, Ibrahim aliwaendea masanamu akayavunja vipande vipande, isipokuwa sanamu kumbwa, hilo aliliacha ili wapate kuliregea waliulize yalio wasibu miungu yao nalo halikujibu kitu, kwa hivyo upotovu wa ibada yao ikabainika.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hapo Ibrãhîm akawavunjavunja masanamu akawafanya vipande vipande vilivyo vidogo na akamuacha mkubwa wao, ili watu wake wapate kumrudia kumuuliza, na ili ulemevu wao na upotevu wao upate kujulikana waziwazi, na ili hoja isimame kwao.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net