Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 21 · Aya ya 31

Al-Anbiyaa 21:31

الأنبياء

وَجَعَلْنَا فِى ٱلْأَرْضِ رَوَٰسِىَ أَن تَمِيدَ بِهِمْ وَجَعَلْنَا فِيهَا فِجَاجًا سُبُلًا لَّعَلَّهُمْ يَهْتَدُونَ

Maana

Na tukaweka katika ardhi milima iliyo thabiti ili isiwayumbishe, na tukaweka humo njia pana ili wapate kuongoka.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na tukaweka katika ardhi milima iliyo thibiti ili isiwayumbishe, na tukaweka humo njia pana ili wapate kuongoka. [31]

[31] Na katika dalili za uweza wetu ni kuwa tumeifanya milima imesimama imara kwenye ardhi ili isiyumbeyumbe nao watu, na tumefanya humo njia pana, za kupitia kwa wasaa, ili waweze kuongoza njia humo kwa makusudio yao. Maoni ya wataalamu juu ya Aya ya 31: "Na tukaweka katika ardhi milima iliyo thibiti ili isiwayumbishe, na tukaweka humo njia pana ili wapate kuongoka." Ilivyo kuwa ndani ya ardhi kila kitu kimeyayuka, na lau kuwa milima imewekwa tu katika baadhi ya sehemu za huu mpira wa dunia kama majabali yaliyo nyanyuka juu tu, uzito wao ungeli sabibisha gamba la dunia liyumbe, au lipindane na kupasuka. Kwa hivyo Mwenyezi Mungu kwa utukufu wa shani yake ameifanya milima isimame imara kwa kuwa na mizizi iliyo zama kwenye gamba la ardhi mpaka chini kwenye kina kirefu kulingana na urefu wake kwendea juu. Kwa hivyo imekuwa hiyo milima kama vigingi, kama alivyo jaalia eneo la minyanyuka hii na mizizi ni duni kuliko maeneo ya gamba lilio zunguka. Yote haya ni kwa ajili ya kueneza sawa uzito wa juu ya gamba kwa pande zote ili pasiwepo kuyumbayumba na kupasuka. Kwani hakika kuenezwa kwa uzito juu ya uso wa dunia yakaribia kuwa hakuleti athari kubwa ya kutajika. Na ilimu za kisasa zimethibitisha kuwa kuenezwa kwa nchi kavu na maji juu ya ardhi, na kuwepo mfululizo wa milima juu yake ni katika yanayo hakikisha hali ilivyo ardhi, na imethibitika kuwa chini ya milima mizito kuna vitu vyepesi kubungunyika, na chini ya maji ya bahari kuu vipo vitu vizito. Kwa kuenezwa uzani wa namna hiyo mbali mbali katika dunia, na mgawanyo huu wa milima, makusudio yake ni kusawizisha uzani wa mpira huu wa ardhi. Na ilivyo nyanyuka milima zikatokea nyanda na mabonde na njia baina ya milima na mwambao na bahari na minyanyuko, na zikawa njia.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na tumeumba kwenye ardhi majabali yenye kuituliza isitikisike na tumetoa, kwenye hayo majabali, njia kunjufu, ili viumbe waongoke kwenye njia za kujitafutia maisha yao na kumpwekesha Muumba wao.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Anbiyaa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net