Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 21 · Aya ya 11

Al-Anbiyaa 21:11

الأنبياء

وَكَمْ قَصَمْنَا مِن قَرْيَةٍ كَانَتْ ظَالِمَةً وَأَنشَأْنَا بَعْدَهَا قَوْمًا ءَاخَرِينَ

Maana

Na ni mingapi katika miji iliyokuwa ikidhulumu tumeiteketeza, na tukawaanzisha baada yao kaumu wengine.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na mingapi katika miji iliyo kuwa ikidhulumu tumeiteketeza, na tukawasimamisha baada yao watu wengine. [11]

[11] Na wengi katika watu wa miji tuliyo iteketeza kwa sababu ya ukafiri wao na kuwakadhibisha Manabii, na baada yao tukasimamisha kaumu nyengine zenye hali bora na mwisho mwema kuliko hao.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na kuna miji mingi ambayo watu wake walikuwa madhalimu kwa kukanusha kwao yale ambayo Mitume wao walikuja nayo. Ndipo tukawaangamiza kwa adhabu iliyowamaliza wote, na tukafanya wapatikane watu wengine wasiokuwa wao.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Anbiyaa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net