Al-Anbiyaa 21:106
الأنبياءإِنَّ فِى هَـٰذَا لَبَلَـٰغًا لِّقَوْمٍ عَـٰبِدِينَ
Hakika katika haya yapo mawaidha kwa watu wafanyao ibada.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hakika katika haya yapo mawaidha kwa watu wafanyao ibada. [106]
[106] Hakika katika haya tuliyo yataja, khabari za Manabii pamoja na kaumu zao, na khabari za Pepo na Moto, yanatosha kuwakumbusha na kuwafanya wazingatie watu walio tayari kumuabudu Mwenyezi Mungu pekee na hawasalitiki na mapambo ya dunia.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Kwa hakika, kwenye mawaidha haya yanayosomwa pana mazingatio ya kutosha kwa watu wenye kumuabudu Allah Mtukufu kwa namna Aliyowawekea na Anayoiridhia kutoka kwao.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net